RC Mtwara: Mtwara iko salama

RC Mtwara: Mtwara iko salama

MTWARA: MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi amewahakikishia wananchi mkoani humo kuwa hali ya usalama kwenye mkoa huo iko shwari na tulivu.

Akizungumza mkoani Mtwara, mkuu huyo wa Mkoa wa Mtwara amesema vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo vinaendelea kuimarisha doria kwa kushirikiana na wananchi.

“Kama tunavyojionea katika mkoa wetu wananchi wetu wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji, kiuchumi na za kijamii”amesema Msengi

Mbali na hilo amezungumzia kuhusu tukio lililotokea Juni 30, 2026 katika Wilaya ya Newala mkoani humo kuhusu kuwepo kwa msuguano uliyotokea kati ya maofisa usafirishaji (maarufu bodaboda) na Jeshi la polisi wilayani humo na kwamba halihusiana na kile kinachoendelea kwenye harakati za mitandao ya kijamii kuhusu maandaano ya Julai 7, mwaka huu kama baadhi ya watu wanavolielezea tukio hilo.

“Tukio hilo halihusianiani kabisa na kinachoendelea kwenye harakati za mitandao ya kijamii kuhusu maandamano ya tarehe 7 Julai mwaka huu kama baadhi ya watu wanavolielezea tukio hili”amesisitiza Msengi

Aliongeza kuwa “Bali ilikuwa ni madai ya kawaida ya maofisa usafirishaji kutaka uhalisia wa tafsiri ya sheria kufuatia kamata kamata ya jeshi letu la polisi, walivyodai hapo awali”

Baada ya tukio hilo wasafirishaji hao walisikilizwa kwenye ngazi ya wilaya kwenye Wilaya hiyo na suala lao hilo tayari kimeshapatiwa ufumbuzi.

Aidha ametoa rai kwa maofisa usafirishaji wote wa vyombo vya moto mkoani humo kufata sheria bila shuruti ili kuhakikisha usalama wa kila mtumiaji wa barabara na kupunguza msuguano baina ya jeshi hilo na wananchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button