PURA yasisitiza uwekezaji sekta ya mafuta na gesi

DAR ES SALAAM: Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mhandisi Charles Sangweni, akishiriki katika Kongamano la Siku ya Nishati (Energy Day) linaloendelea katika Ukumbi wa Mwandoro, Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba, jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Sangweni ameeleza kuhusu nafasi ya sekta ya mafuta na gesi asilia katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa, pamoja na umuhimu wa usimamizi na udhibiti wa shughuli za mkondo wa juu wa petroli.

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuvutia uwekezaji, kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali pamoja na kutumia fursa zilizopo katika sekta ya mafuta na gesi kwa manufaa ya taifa.

Kongamano hilo limewakutanisha viongozi, wataalam, wawekezaji, washirika wa maendeleo na wadau wengine wa sekta ya nishati kujadili mwelekeo wa sekta, fursa za uwekezaji, ubunifu na teknolojia kwa maendeleo ya Tanzania.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button