Shule ya Msingi Mwananyamala B yakabidhiwa madawati

Klabu ya Rotary imekabidhi madawati 150 kwa Shule ya Msingi Mwananyamala B, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa kuboresha mazingira ya kujifunzia na kujifunza kwa wanafunzi pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuinua kiwango cha elimu nchini.

Akizungumza katika makabidhiano hayo leo Aprili 29, Ofisa Elimu wa Kata ya Makumbusho, Mwalimu Simon Mirobo, amepongeza msaada huo akisema utasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati na kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora na rafiki.

Naye, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwananyamala B, Modesta Mushi, amesema msaada huo utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji shuleni.

Kwa upande wake, Rais wa Rotary Club Dar es Salaam, Lenali Munyua, amesema Rotary itaendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha sekta ya elimu na ustawi wa jamii.

 

Aidha, Mwenyekiti wa Rotary Tanzania, Ambrose Ntageki, pamoja na Gavana wa Kanda, Daniel Mukasa Damulila, wamesema Rotary itaendelea kuhamasisha wanachama wake kushiriki katika miradi ya kijamii yenye manufaa kwa wananchi, hususan katika sekta ya elimu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button