Muswada kufuta sheria tasnia ya pareto wawasilishwa bungeni

DODOMA; Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo leo Agosti 28, 2026 amewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Kufuta Sheria ya Tasnia ya Pareto wa Mwaka 2026.

“Lengo la kufutwa kwa Sheria hii ni kuendeleza juhudi za Serikali za kupunguza gharama za uendeshaji kwa kuunganisha taasisi mbalimbali zinazotekeleza majukumu yanayofanana kwa lengo la kupunguza wingi wa taasisi za udhibiti kwa shughuli zinazofanana, kuimarisha uratibu, kuongeza ufanisi na kuhakikisha matumizi yenye tija ya rasilimali za umma katika sekta ya kilimo.

“Muswada huu umegawanyika katika sehemu mbili, ambapo sehemu ya kwanza inahusu masharti ya utangulizi, ikijumuisha jina la muswada na fasili ya misamiati mbalimbali iliyotumika katika muswada.

“Sehemu ya Pili ya Muswada inaweka masharti kuhusu kufutwa kwa Sheria ya Tasnia ya Pareto pamoja na masuala ya mpito, ambapo majukumu, mali, madeni pamoja na watumishi wa Bodi ya Pareto wanahamishiwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko.

“Lengo la kufuta Bodi ya Pareto ni kupunguza wingi wa taasisi za udhibiti kwa shughuli zinazofanana, kuimarisha uratibu, kuboresha usimamizi wa udhibiti na kuhakikisha matumizi yenye tija ya rasilimali za umma katika sekta ya kilimo,” amesema Waziri Chongolo

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

  2. Wonderful beat ! I wish to apprentice while you amend
    your site, how could i subscribe for a blog site? The
    account aided me a acceptable deal. I had been tiny
    bit acquainted of this your broadcast provided bright clear idea

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button