Jaydee: Wanawake wasihukumiwe kwa mavazi

DAR ES SALAAM: Msanii wa muziki wa bongo fleva Judithi Wambura ‘Lady Jaydee’, ameitaka jamii kuacha kuhukumu wanawake kwa namna wanavyovaa, akisema mavazi ya mtu hayapaswi kutumika moja kwa moja kupima tabia yake.

Akizungumza na DailyNews Digital, Lady Jaydee amesema baadhi ya watu huvaa kwa sababu wanapenda mtindo huo, kwa ajili ya kazi au kujieleza kisanii, hivyo jamii inapaswa kutenganisha mavazi na tabia.

Amesema kila mtu ana uhuru wa kujieleza kwa namna yake, mradi anazingatia mazingira anayokuwamo.

“Tabia sio nguo,” amesema, akisisitiza kuwa jamii inapaswa kuwapa wanawake nafasi na uhuru wa kujieleza bila kuwahukumu kwa mavazi yao.

Amesema suala la mavazi linapaswa pia kuangaliwa kwa kuzingatia mazingira, akitoa mfano wa mtu anayekwenda benki ambaye anapaswa kuzingatia aina ya mavazi yanayofaa kwa mazingira hayo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button