Verto, Visa wapania kuongeza ufanisi malipo kimataifa

DAR ES SALAAM; Kampuni ya kimataifa ya teknolojia ya fedha, Verto, kwa kushirikiana na Visa, imezindua kadi maalumu ya biashara inayojumuisha sarafu nyingi kuwezesha malipo ya kimataifa.

Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi Mwenza wa Verto, Ola Oyetayo, alisema huduma hiyo inalenga kukabiliana na pengo kubwa la miundombinu ya kifedha linalozikabili biashara za barani Afrika zinazofanyika kimataifa.

Amesema kadi hiyo inalenga kusaidia wafanyabiashara barani Afrika kupunguza gharama za ubadilishaji wa fedha za kigeni, kuboresha usimamizi wa matumizi ya fedha na kuongeza ufanisi wa shughuli zao katika masoko ya kimataifa.

“Biashara za Afrika zimekua na kuvuka mipaka kwa kasi kikubwa kuliko miundombinu ya kifedha inayozihudumia. Kwa sasa, changamoto si upatikanaji wa masoko, bali ni namna fedha zinavyohamishwa.

“Kampuni nyingi bado zinapoteza fedha kutokana na gharama zisizo za lazima katika ubadilishaji wa fedha, ucheleweshaji wa malipo na taratibu za kibenki zilizogawanyika, ambazo huathiri moja kwa moja faida na ukuaji wa biashara.

“Kadi ya Verto imeundwa kuwapa wafanyabiashara udhibiti mkubwa zaidi wa matumizi ya kimataifa, huku ikipunguza baadhi ya vikwazo ambavyo kwa muda mrefu vimeambatana na biashara hizo kimataifa,” amesema na kuongeza:

“Uzinduzi huo unafanyika wakati ambapo biashara zinazidi kupanua shughuli zao katika masoko mbalimbali, hali inayoongeza mahitaji ya kadi ya sarafu nyingi inayowawezesha kutumia Dola za Marekani (USD), Canada (CAD), Australia (AUD),  New Zealand (NZD) pamoja na Euro ya Ulaya
(EUR).

“Au  Yen ya Japan (JPY), Pauni ya Uingereza (GBP), Faranga ya Uswisi (CHF), Krone ya Norway (NOK) na Krona ya Sweden (SEK) bila kulazimika kuhamisha fedha au kulipa gharama za ziada wakati wa ubadilishaji wa fedha,” amesema.

Kwa upande wake Shahebaz Khan, ambaye ni Makamu wa Rais Mwandamizi na Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Uhamishaji Fedha wa Visa, amesema
jukwaa hilo linajumuisha pia mifumo ya kudhibiti matumizi, utoaji wa kadi papo hapo na usalama wa miamala ulioimarishwa.

“Usimamizi wa sarafu nyingi haupaswi kuwa kikwazo cha ukuaji kwa biashara zinazolenga kupanua shughuli zao kimataifa.

“Ushirikiano wetu na Verto unasaidia kurahisisha namna biashara zinavyowalipa wasambazaji, kusimamia gharama na kufanya miamala kimataifa huku zikipata usalama na ukubalifu mpana wa
kimataifa wanaoutegemea kutoka Visa,” alisema Khan.

Amesema Visa inaamini kuwa uchumi unaojumuisha kila mtu na kila mahali, humuinua mtu yeyote popote alipo na kwamba upatikanaji wa huduma za kifedha ni msingi muhimu wa mustakabali wa uhamishaji wa fedha.

Kadi hiyo ya Verto inawawezesha wafanyabiashara kutumia fedha moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao bila kulazimika kuhamisha fedha kati ya akaunti ama kubadilisha fedha kabla ya kufanya
malipo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Home cash earning job to earns more than $220 per Hour!** getting paid weekly more than 4700+Dollar per week or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. **Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA…
    .
    Here is I started_____ ⫸ http://Www.Cash54.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button