Zaidi ya watu 300 kushiriki mkutano wa vijana

DAR ES SALAAM: ZAIDI ya watu 300, wakiwemo vijana, viongozi wa Serikali, watunga sera, wataalamu wa afya, mashirika ya kiraia na wadau wa maendeleo, wanatarajiwa kushiriki Mkutano wa Young and Alive Summit 2026 unaolenga kutoa nafasi kwa vijana kujadili changamoto zao na kushiriki katika kutafuta suluhisho.

Mkutano huo utafanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 14, mwaka huu katika Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ukiwa na kaulimbiu “From Voices to Action: Taking Young People as Drivers for Accountability for Inclusive Health and Wellbeing.”

Akizungumza kuhusu mkutano huo, Mratibu wa Mradi huo Cecilia Lubango amesema jukwaa hilo lilianzishwa mwaka 2022 kwa lengo la kuwaunganisha vijana, viongozi wa vijana, watunga sera, Serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wa maendeleo.

Amesema mkutano huo unalenga kuwapa vijana nafasi ya kujifunza, kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto zinazowakabili na kushiriki katika kuandaa suluhisho zinazoweza kuleta mabadiliko katika jamii.

“Katika mkutano wa mwaka huu kutakuwa na mijadala na shughuli mbalimbali zitakazojikita katika afya ya uzazi, vijana na uongozi, usawa wa kijinsia na afya ya akili.

Amesema baadhi ya washirika tayari wamejitolea kutoa huduma wakati wa mkutano huo, ikiwemo uchunguzi wa afya ya akili utakaofanywa na wataalamu wa saikolojia, pamoja na uchunguzi wa ugonjwa wa selimundu unaotarajiwa kufanywa na Ruge Mutabazi Foundation.

Kwa upande wake Kelvin Melisi, mwakilishi wa vijana atakayeshiriki , amesema mtandao huo unaunganisha vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini na unalenga kuhakikisha wanapata taarifa sahihi kuhusu afya, afya ya akili, uchumi na ujasiriamali.

Amesema Young and Alive Summit ni fursa muhimu kwa vijana kukutana na viongozi wa Serikali, watunga sera, wataalamu na watoa huduma mbalimbali ili kupata taarifa na kujadili changamoto zinazowakabili.

“Tunahitaji vijana wajitokeze kwa wingi kwa sababu huu ni mkutano unaotupa nafasi ya kujifunza, kuungana na kuchukua hatua. Kama tunasema From Voices to Action, basi tusibaki kusema tu, tutoke na tufanye kwa vitendo,” amesemi

Amewataka vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini kutumia fursa hiyo kujifunza na kuibua changamoto zinazowakabili, akisema ushiriki wao ni muhimu katika kuhakikisha mahitaji yao yanafika kwa wahusika wenye uwezo wa kuchukua hatua.

Naye Amboki Nyangala, kijana mwenye ulemavu na mshiriki wa Young and Alive Summit 2026, amesema jukwaa hilo ni muhimu kwa kuwa linatoa nafasi kwa vijana wenye ulemavu kushiriki katika mijadala inayohusu ustawi wao.

Amesema vijana wenye ulemavu wana haki ya kupata elimu na huduma za afya ya uzazi kama vijana wengine, hivyo ni muhimu kusikiliza maoni yao na kuzingatia mahitaji yao katika mipango na huduma zinazowahusu.

Nyangala amesema mkutano huo utawapa vijana kutoka mikoa mbalimbali nafasi ya kukutana, kubadilishana mawazo na uzoefu, pamoja na kujadili changamoto zao kwa pamoja.

Amesema ushirikishwaji wa vijana wote, wakiwemo wenye ulemavu, utasaidia kujenga jukwaa linalozingatia mahitaji mbalimbali na kuwezesha vijana kushiriki katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button