Madereva wanawake wahimizwa mbio za magari

MOROGORO: MKUU wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala ametoa hamasa kwa  wanawake nchini ambao ni madereva kujitokeza kwa wingi kushiriki mchezo wa mashindano ya mbio za magari  kama ilivyo kwenye michezo mingine ili kuleta ushindani  .

Kilakala ametoa wito huo wakati akizundua mashindano ya mbio za magari ya Serengeti Rally Tanzania 2026  yaliyoanza Oktoba  Mosi na kufikia  tamati Oktoba 4, 2026  kwenye  shamba la  miti  la  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), mkoani Morogoro.

Mashindano hayo yanayoshirikisha madereva 24 kutoka ndani na nje ya Tanzania na  miongoni mwao tisa wanashiriki kuwania ubingwa wa African Rally Championship , na wengine  wakiwania ubingwa wa ndani.

“ Nichukue fursa hii niwahamasishe wanawake amba oni madereva kujitokeza kwa wingi kushiriki mchezo huo “ amesema Kilakala.

Katika mashindano hayo mwanamke  Susan Muwonge, ndiye pekee aliyejitosa kushiriki kwenye mashindano hayo akiwakilisha nchi  yake ya Uganda  akiwania  ubingwa wa African Rally Championship.

Mkuu wa wilaya pia amewataka watazamaji kuzingatia usalama wakati wote wa mashindano na umuhimu wa kutunza mazingira ili  shughuli zao zisiathiri uoto wa asili wa Msitu wa Shamba la Miti Morogoro.

Kilakala pia  amesisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na  kuhakikisha shughuli zao haziathiri uoto wa asili na mazingira.

Naye, Msimamizi Mkuu wa mashindano hayo, Dk Mosi Makau amesema mashindano hayo yanaleta  fursa na kuongeza uchumi kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro.

Kwa upande wake Naibu Kamishna wa Uhifadhi na Mkurugenzi wa Uzalishaji Mbegu za Miti TFS, Dk Hamza Katety  amesema Wakala huo utaendelea kusimamia na kulinda mazingira ambayo ni sehemu muhimu ya kuwezesha shughuli mbalimbali kufanyika katika maeneo ya misitu.

Dk Katety amehimiza  wananchi kutumia fursa hiyo pia kujifunza na kufanya utalii wa ikolojia, kwa kutembelea hifadhi na maeneo mbalimbali ya asili yanayopatikana mkoani Morogoro ambayo yanasimamiwa na  Wakala huo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button