Saikolojia nyuma ya maamuzi ya kufanya biashara

DAR ES SALAAM; Hali ya kiakili inaweza kubadilisha namna mtu anavyotenda na kutafsiri taarifa. Katika makala ya leo, tungependa kujadili mambo 4 ya kisaikolojia yaliyoenea zaidi ambayo mara nyingi huathiri mchakato wa kufanya maamuzi kwa wafanyabiashara.

Hasa, tutaangazia jukumu la hofu, kujiamini kupita kiasi, kukosa subira, na hofu ya kupata hasara katika masoko pamoja na njia za kukabiliana navyo.

Hofu na Msukumo wa Kufanya Jambo Fulani

Hofu ni mwitikio wa kawaida kwa jambo lisilojulikana. Katika soko la hisa, inaweza kuchochewa na matukio yasiyotarajiwa au kushuka kwa thamani ya nafasi (position) ya mtu sokoni.

Wakati mwingine hofu inaweza kuwafanya wafanyabiashara kufunga nafasi zao kabla ya wakati, kupuuza fursa zenye faida zinazoendana na mkakati wao, au kuchukua hatua za ghafla kwa kutumia taarifa zisizokamilika.

Katika hali nyingine, hofu ya kuachwa nyuma (FOMO) inaweza kuwalazimu wafanyabiashara kuingia sokoni kwa sababu tu ya bei zinazobadilika kwa kasi.

Kinachosaidia: Kutambua hisia kama hizo hakuzuii zisitokee, lakini kunaweza kusaidia kukabiliana nazo vizuri zaidi.

Kujiamini Kupita Kiasi Baada ya Mafanikio

Mfululizo wa biashara zenye faida unaweza kuongeza kiwango cha kujiamini. Ingawa hisia hii ina manufaa, ikizidi kiasi huwa na mwelekeo wa kuwafanya wafanyabiashara kupuuza hatari (risks).

Wafanyabiashara wanaweza kuishia kuchukua nafasi kubwa zaidi, kufanya biashara mara kwa mara, na kutotumia uchambuzi baada ya kupata ushindi mara chache.

Kinachosaidia: Kusoma nyenzo za kielimu mara kwa mara na kufanya biashara kwenye akaunti ya majaribio (demo) kwanza ili kujifunza zaidi jinsi masoko yanavyofanya kazi na jinsi ya kufanya biashara badala ya kutegemea biashara moja iliyofanikiwa.

Unaweza kupata huduma zote mbili kwenye jukwaa la biashara la JustMarkets. Nyenzo za kielimu zinajumuisha uchambuzi wa kila siku, Kalenda ya Kiuchumi, makala za biashara, video, faharasa ya maneno, utabiri wa soko, machapisho ya Kituo cha Usaidizi, na mengine mengi.

Kukosa Subira na Kufanya Maamuzi ya Ghafla

Fursa hazijitokezi mara moja kila wakati ndani ya soko. Kwa njia hii, inaweza kuwa vigumu kusubiri fursa zinazokidhi vigezo vya biashara vilivyowekwa na mfanyabiashara.

Tatizo hapa ni kwamba mtu anaweza kuishia kufanya biashara bila kufanya uchambuzi wa aina yoyote au kuendelea kuingia na kutoka kwenye biashara ili tu kuonekana yuko bize.

Kinachosaidia: Kuwa na miongozo iliyowekwa kuhusu jinsi ya kuingia na kutoka sokoni kunaweza kusaidia katika kukabiliana na maamuzi ya ghafla kama hayo.

Hofu ya Kupata Hasara (Loss Aversion)

Utafiti katika uchumi wa kitabia umeonyesha kuwa watu mara nyingi hupata athari ya kisaikolojia kutokana na hasara kwa nguvu zaidi kuliko faida zinazolingana. Katika biashara, mwelekeo huu unajulikana kama loss aversion.

Unaweza kuwashawishi wafanyabiashara kushikilia nafasi zinazoingiza hasara kwa muda mrefu wakitarajia kuwa bei zitarejea, huku wakifunga nafasi zenye faida haraka mno ili kulinda faida. Maamuzi yote mawili yanaweza kuongozwa zaidi na hisia kuliko mpango wa awali wa biashara.

Kinachosaidia: Kuweka shajara ya biashara (trading journal) kunaweza kuwasaidia wafanyabiashara kutambua mifumo ya tabia inayojirudia na kukagua kama maamuzi yalitokana na uchambuzi au miitikio ya kihisia.

Kujijengea Uelewa Binafsi

Kufanya maamuzi yenye mafanikio kunavuka mipaka ya kutabiri mwenendo wa soko na kunahitaji uelewa wa jinsi watu binafsi wanavyoitikia hatari, kutokuwa na uhakika, faida, na hasara.

Mipango ya biashara, viwango vya hatari vilivyoainishwa awali, shajara za biashara, na tathmini za utendaji ni miongoni mwa mambo yanayoweza kuleta uelewa binafsi.

Majukwaa ya biashara kama vile JustMarkets yanawapa watu njia mbalimbali za kufanya biashara na kujifunza, na hivi ndivyo maendeleo yanavyopatikana.

Onyo la Hatari: Kufanya biashara ya Forex na CFDs kunahusisha hatari kubwa na kunaweza kusababisha kupoteza mtaji wako uliowekeza. Nyenzo hii ni kwa ajili ya kutoa taarifa pekee na haijumuishi ushauri wa uwekezaji.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button