Kuzaga awasisitiza polisi kata nidhamu, uadilifu

MBEYA: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga, amewataka Polisi Kata mkoani humo kuzingatia nidhamu, weledi na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuleta matokeo chanya kupitia falsafa ya Polisi Jamii.
Wito huo ameutoa Novemba 17, 2026, wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki nne kwa ajili ya kuimarisha utendaji wa Polisi Kata na vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Pikipiki hizo zimekabidhiwa kwa Polisi Kata za Busale na Talatala zilizopo Wilaya ya Kyela, Polisi Kata ya Lualaje iliyopo Wilaya ya Chunya pamoja na kikundi kimoja cha ulinzi shirikishi cha Kata ya Talatala.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kuzaga amewataka Polisi Kata kuzitumia pikipiki hizo kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi, kutoa elimu na kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii katika masuala ya ulinzi na usalama.
Aidha, amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, kwa kutoa pikipiki tatu, huku akimpongeza mdau mmoja aliyetoa pikipiki nyingine kwa ajili ya Polisi Kata ya Lualaje baada ya kuvutiwa na utendaji kazi wake.
Amesema msaada huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuongeza uwezo wa kiutendaji wa Polisi Kata katika kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kyela, Mrakibu wa Polisi (SP) Salehe Njama, ameahidi kuendelea kuwasimamia Polisi Kata kwa karibu, kuhakikisha pikipiki hizo zinatunzwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Amesema usimamizi huo utalenga kuhakikisha vifaa hivyo vinachangia kuboresha utekelezaji wa majukumu ya Polisi Kata kama ilivyokusudiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.
Naye, Kiongozi wa Kikundi cha Ulinzi Shirikishi cha Kata ya Talatala, Mohamed Kasinde, amesema pikipiki hiyo itaongeza ufanisi katika shughuli za kuzuia na kutanzua uhalifu.
Ameahidi kuwa kikundi hicho kitaendelea kufanya kazi kwa bidii na uadilifu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha usalama wa wananchi.




NEW88.COM – Nhà Cái Giải Trí Trực Tuyến Hàng Đầu, Mang Đến Trải Nghiệm Cá Cược Đẳng Cấp Với Kho Game Đa Dạng tại: https://rtsjhsrgse.sa.com