Afcon 2027 itaeneza Kiswahili duniani- Makonda

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) itakuwa sehemu ya juhudi za kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili duniani.

Makonda amesema matumizi ya Kiswahili katika michuano hiyo yanaweza kuongeza wigo wa lugha hiyo kimataifa, akieleza kuwa Kiswahili ni lugha adhimu inayounganisha watu na mataifa mbalimbali na kujenga mshikamano.

Ametoa kauli hiyo leo, Novemba 25, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kukabidhi ofisi kwa Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) nchini Tanzania, katika maandalizi ya michuano ya AFCON 2027.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button