FFC, wafanyabiashara wajadili changamoto

WADAU wa biashara mbalimbali nchini wamekubaliana kwa pamoja kuhakikisha bidhaa wanazoagiza kutoka nje zinakuwa na chapa ya nchi zilizotengenezwa ili kulinda soko lao na kuepuka utengenezaji wa bidhaa bandia.

Wakizungumza leo Januari 28, 2023 Makao Makuu ya Tume ya Ushindani (FCC) baadhi ya wafanyabiashara wamesema hatua hiyo itawafanya kuondokana na vikwazo mbalimbali ambavyo wamekuwa wakikutana navyo wakati wa uingizwaji wa bidhaa nchini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Spanish Tiles & Sanitary Ware, Rohit Siwach ameshauri  kila bidhaa inayoagizwa kutoka nje iwe na chapa kwenye boksi au ndani ya bidhaa na ikibidi kuwe na ‘video’ ya ushahidi inayoonyesha jinsi bidhaa hiyo ilivyotengezwa.

“Nadhani kuna haja wakati wa utengenezaji kuwe na video kiwandani inayoonyesha namna wanavyotengeneza itasimama kama ushahidi.” amesema Siwach.

Mfanyabiashara wa Nordic Computer Limited, Chris Adler ameshauri kuwa tume hiyo inapaswa kufanyakazi kwa ukaribu na Shirika la Viwango nchini (TBS) ili kuwalinda wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa nje ya nchi.

Katika kikako hicho kilichokutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, baadhi yao wameshauri endapo kutakuwa na bidhaa bandia kutoka nje ambayo imejumuishwa kwenye bidhaa halali basi iondolewe bidhaa hiyo feki ikiwezekana kupigwa fainai na halali iruhusiwe.

Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio amewashauri wafanyabiashara kuzingatia sheria za uingizaji wa biashara na kuwashauri wateja ili kuepuka sintofahamu ya ushikiliwaji na utengenezaji wa bidhaa bandia.

“Kwanza tumekubaliana wahakikishe bidhaa inaonesha imetoka wapi, na kuangalia aina ya bidhaa pia wapi imetengenezwa.” amesema Erio.

Ameongeza kuwa katika kulipatia ufumbuzi suala hilo, wamepanga kufanya mkutano mwingine katikati ya mwezi Februari  utakaokutanisha wadau mbalimbali wa biashara ili kufikia mwafaka wa jambo hilo.

Mwakilishi wa wafanyabiashara, Baraka Mase amesma tatizo la uingizaji wa bidhaa bandia unatokana na uwepo wa mikapa halali na isiyo halali ambayo baadhi wa watu wamekuwa wakiitumia kwa lengo la kuingiza bidhaa zao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button