Naibu Waziri apatiwa maelezo juu ya Afya Mkopo

Dodoma: Naibu Waziri wa afya Dk Florence Samizi akimsikiliza Mkuu wa kanda ya kati Vodacom Tanzania Plc Chiha Nchimbi (katikati) aliyekuwa akifafanua jambo juu ya mikopo kwa watoa huduma binafsi wa sekta ya afya.
Naibu Wiziri ni miongoni mwa viongozi wa serikali waliotembelea banda la Afya Mkopo katika kongamano la wadau wa sekta ya afya binafsi linaloendelea jijini Dodoma.
Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na PharmAccess Foundation kupitia Medical Credit Fund wanatoa huduma ya mikopo kwa watoa huduma binafsi wa sekta ya afya ambao hupatiwa mikopo kwa haraka, kwa urahisi na kwa masharti nafuu ili kupanua huduma, kuboresha miundombinu na kukuza biashara zao.
Kushoto kwake ni Dk Heri Marwa Mkurugenzi wa PharmAccess Foundation na kulia ni Maula Mafuru Meneja mauzo wa M-Pesa kanda ya kati



