Polisi Arusha wakamata sikaha, risasi 71
Jeshi la Polisi mkoani Arusha, limefanikiwa kukamata bastola moja aina ya CZ 75 LUGER yenye namba za usajili A487385, pamoja na risasi 71 za bastola iliyokuwa inatumiwa na wahalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo amesema silaha hiyo pamoja na risasi zilipatikana katika nyumba iliyopo huko maeneo ya Ilkyurei, Kata ya Kiranyi, Wilaya ya Arumeru.
Amefafanua kuwa wahalifu hao walikimbia baada ya polisi kukaribia kufika katika nyumba hiyo na wanaendelea kufanya upelelezi, ili kuwakamata.



