Makonda ataka mikakati ya habari Dira 2050

SERIKALI imeagiza vyombo vya habari viweke mikakati itakayowezesha nchi kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 ya kuwa na uchumi wa dola za Marekani trilioni moja ifikapo 2050.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda alisema hayo katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani jijini Arusha jana.
“Tunayo dira ya taifa ya 2050, tutengenezeni mkakati wa kuwa injini tutakayoifikisha taifa letu kwenye huo uchumi tunaotamani kuufikia…ndugu zangu wanahabari taifa hili halitafikia huo uchumi kama ninyi mkikaa nyuma,” alisema Makonda.
Pia alivitaka vyombo vya habari kuitangaza nchi kwenye utalii, kilimo na sekta nyinginezo na visibaki nyuma kuandika habari njema na kuwajenga waandishi katika taaluma mahususi kama vile utalii, kilimo, mahakama na nyinginezo.
Sambamaba na hilo, Makonda aliwataka waandishi wa habari kujenga uchumi wao imara ili kuwa na uhuru ndani ya vyombo vya habari.
Makonda alisema ni ngumu kupata uhuru wa vyombo vya habari kama waandishi wa habari hawana uwezo wa kiuchumi utakaowaondoa katika kufanya kazi kwa hofu na masimango.
“Uchumi wa wanahabari unapokua mdogo unawapa nafasi wanasiasa uchwara na wala rushwa kuwaweka mfukoni…kuna watu ukiwatazama kwa jicho la habari na namna chombo cha habari kilivyowatengeneza ni watu wema sana, lakini ni wauza dawa za kulevya, wala rushwa wakubwa wazembe, mafisadi, lakini wamefanikiwa kuwakamata wanahabari,” alisema Makonda.
Alihimiza waandishi wa habari watumie vyanzo vya habari vya kuaminika ili wanapoandika habari waandike habari sahihi na sio kuzua taharuki pamoja na kuwa makini katika uandishi ili kuepuka kuandika taarifa ambazo sio sahihi.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Gerson Msigwa alisema lengo la maadhimisho hayo ni kutathimini na kulinda hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini.
Msigwa alisema kupitia maadhimisho hayo serikali inapata fursa kukutana na vyombo vya habari na kujadili mabadiliko ya utendaji, usawa wa kijinsia ndani na nje ya vyombo vya habari, usalama wa wanahabari na kuwaendeleza watengeneza maudhui.



❤️Artificial Intelligence Based S-e-x Game. See –> https://da.gd/Eroplay