Amuua mwenzake kwa kuombwa maji

JESHI la Polisi mkoani Tanga linamshikilia Hassan Nyundo kwa kumchoma kisu mwenzake katika  majibizano.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Henry Mwaibambe alimtaja marehemu kuwa ni Amir Mohamed, mkazi wa Vue, Kata ya Moa wilayani Mkinga kuwa alipatwa na mauti Aprili 5, mwaka huu.

“Mpaka sasa kuna taarifa mbili juu ya tukio hili ambapo wengi wakisema juu ya mtuhumiwa kuchukizwa na kitendo cha marehemu kumwomba maji pamoja na kunywa maji mchana wa mwezi mtukufu wa Ramadhani huku wengine wakisema ni ugomvi wa kawaida,” alisema.

Kamanda Mwaibambe alisema polisi inatarajia kumfikisha mahakamani mtuhumiwa mara tu upelelezi kuhusu tukio hilo utakapokamilika na mwili wa marehemu umeshakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Vilevile Kamanda Mwaibambe aliiasa jamii kutojichukulia hatua za kisheria kinyume na utaratibu hali ambayo inasababisha madhara na kuwa kama kuna sintofahamu miongoni mwao wazifikishe kwenye vyombo vya kisheria ili kutafuta ufumbuzi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button