MWANAFUNZI wa Shahada ya Uzamivu wa Sayansi ya Mazingira katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi ya Nelson Mandela, Aziza Konyo, amebuni uchafu unaozalishwa na zao la mkonge kuwa chakula cha mifugo.
Akizungumza kwenye maonesho ya wakulima Kanda ya Kaskazini yanayoendelea viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha, Aziza amesema tafiti zilizofanyika zimebaini kuwa asilimia nne hadi sita ya zao la mkonge ni kamba zile nyeupe, lakini asilimia kubwa iliyobaki ni uchafu.

Amesema uchafu mwingi unaozalishwa katika zao la mkonge na unaleta athari za kimazingira na kibinadamu, hivyo katika kuondoa tatizo hilo wanatumia teknolojia ya nzi chuma yenye uwezo wa kuchakata uchafu.
“Kama unakilo 100 za taka nzi chuma hao wana uwezo wa kuchakata ndani ya siku 10 hadi 14 zikabaki kilo 20 hadi 40,” amesema.

Amesema ndani ya siku hizo watawavuna nzi nchuma hao kwa ajili ya kuwaandaa kwa chakula cha kuku na samaki na asilimia 2O ya mkonge iliyobaki haitupwi bali itatumika kama mbolea nzuri kwa ajili ya mazao ya mbogamboga zisizo na kemikali.
Back to top button