Serikali iwekeze nguvu watumishi TAEC

ARUSHA; KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), imeiomba serikali kuajiri watumishi wa kutosha, kwenye Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), ili kuendana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika maabara ya kisasa iliyogharimu Sh bilioni 10.
4
Ombi hilo limetolewa jijini Arusha na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Augustine Holle ambaye amesema wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.

“Huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali yetu, hivyo sisi kama kamati tutaiomba serikali kuongeza watumishi zaidi, ili kuendana na uwekezaji huu wa kisasa na wa kihistoria,” amesema.
Amesema maabara hiyo ina vifaa vya kisasa,hivyo vizuri kuwepo watumishi wengi na wenye ujuzi wa kufanya kazi katika maabara hiyo, ili lengo la serikali litimie la kuwa na maabara yenye tija kwa Taifa na nje ya nchi.

Awali Mkurugenzi wa TAEC Profesa Lazaro Busagala, amesema ili kuwasogezea karibu wananchi huduma zao, wameanzisha kanda saba.



