Serikali iwekeze nguvu watumishi TAEC

ARUSHA; KAMATI ya Kudumu ya Bunge  ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC),  imeiomba serikali kuajiri watumishi wa kutosha, kwenye Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC),  ili kuendana na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika maabara ya kisasa iliyogharimu Sh bilioni 10.4

Ombi hilo limetolewa jijini Arusha na Mwenyekiti wa kamati hiyo,  Augustine Holle ambaye amesema wameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.

“Huu ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali yetu, hivyo sisi kama kamati tutaiomba serikali kuongeza watumishi zaidi, ili kuendana na uwekezaji huu wa kisasa na wa kihistoria,” amesema.

Amesema maabara hiyo ina vifaa vya kisasa,hivyo vizuri kuwepo watumishi wengi na wenye ujuzi wa kufanya kazi katika maabara hiyo, ili lengo la serikali litimie la kuwa na maabara yenye tija kwa Taifa na nje ya nchi.

Awali Mkurugenzi wa TAEC  Profesa  Lazaro Busagala, amesema ili kuwasogezea  karibu  wananchi huduma zao, wameanzisha kanda saba.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Marry
Marry
1 month ago

[Be Your Own Boss] Work online from home and earn over $15,000 just by doing an easy job. Last month I earned and received (xN)$20,000 from this job doing an easy part time job. j In fact, this job is so easy to do and regular income is much better than other normal office jobs where you have to deal with your boss…. 
HERE →→→→→→ http://www.smartcareer1.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x