Wafanyabiashara Tanga waomba kuboreshewa soko

WAFANYABIASHARA wa Soko Kuu la Mgandini jijini Tanga wameiomba Halimashauri ya Jiji la Tanga kuwaboreshea miundombinu ya soko ili kufanya shughuli zao katika mazingira mazuri.

Wakizungumza katika kikao chao na mkurungenzi wa jiji hilo, Said Majaliwa cha kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao.

Walisema kuwa uchakakavu wa miundombinu ikiwemo mifumo ya majitaka imekuwa ikihatarisha hali za afya za wafanyabiashara hao pamoja na watumiaji wengine wa soko hilo Kwa ujumla.

Mmoja wa wafanyabiashara hao Elizabeth Sozi alisema kuwa licha ya kutozwaa ushuru na halmashauri hiyo lakini swala la miundombinu limekuwa changamoto hasa nyakati za mvua.

“Nyakati za mvua hapa sokoni huwezi kuuza kwani miundombinu ni chakavu tunaomba tuboreshewe Ili tuweze kufanyabiashara katika mahali pazuri”alisema Soza.

Hata hivyo Mkurungenzi wa Jiji la Tanga Said Majaliwa alisema kuwa soko hilo lipo kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa na kuwa la kisasa.

“Niwaombe wafanyabiashara tuwe na subra kwani serikali imeshaleta kiasi cha Sh bilioni 8 kwa ajili ya kufanya maboresho ya miundombinu na ukarabati mwingine katika soko hilo.”alisema mkurungenzi huyo.

Aidha alisema kuwa katika kutatua kero zilizopo wamejipanga kufanya marekebisho madogo ya miundombinu Ili wafanyabiashara waweze kufanya shughuli zao kwenye mazingira mazuri wakati tukisubiri ukarabati mkubwa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button