Simba inaitaka robo CAF
SIMBA SC imefikisha pointi sita katika msimamo wa Kundi B Ligi ya Mabingwa Afrika, kufuatia sare ya bila kufungana waliyoipata leo dhidi ya Asec Mimosas.
Pointi hizo zinaendelea kuiweka timu hiyo nafasi ya pili katika msimamo wa kundi hilo.
Simba atamaliza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Jwaneng Galaxy mwezi Machi.
Asec inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 11, Simba nafasi ya pili pointi 6, Jwaneng pointi 4 na Wydad pointi 3.



