Samia atengua vigogo TTCL, Posta, UCSAF

DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi sita akiwemo Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta nchini Bw. Maharage Chande.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imetaja viongozi waliofutwa kazi kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bi Zuhura Sinare Muro,  na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Peter Ulanga.

Pia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania, Brigedia Jenerali Mstaafu Yohana Ocholla Mabongo,  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Prof. John Nkoma,  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko Bi. Justina Mashiba.

SOMA: Rais Samia awafuta kazi Makamba, Nape

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Habari Zifananazo

Back to top button