Uganda yapewa mkopo dola miiioni 600

UGANDA : BENKI ya Dunia (WORLD BANK) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) zimetangaza kuipa Uganda mkopo wa zaidi ya dola milioni 600 kwa ajili ya miradi ya miundombinu na usimamizi wa taka jijini Kampala.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na serikali ya Uganda pamoja na Benki ya Dunia dola milioni 566 ni mkopo kutoka Benki ya Dunia na dola milioni 42.7 zitatolewa na AFD.
Mkopo huo umetolewa wakati raia wa Uganda wakilalamikia usimamizi wa takataka na barabara mbovu za mji mkuu, kutokana na bajeti na kutengwa kwa bajeti ndogo na serikali ya Uganda.
SOMA: Tanzania, India kurejeleza taka ngumu
Mwezi uliopita, maporomoko ya takataka yalifukia makaazi ya watu nje kidogo ya mji wa Kampala, na k usababisha vifo vya watu 35.



