Guterres aonya mauaji wafanyakazi UN

MAREKANI : KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mauaji ya wafanyakazi sita ya shirika la wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, katika mashambulizi ya Israel dhidi ya shule iliyogeuzwa hifadhi Gaza.
Mashambulizi hayo yalilenga shule inayohifadhi familia na wapalestina waliopoteza makaazi yao pamoja na kaya mbili, na kuuwa dazeni kadhaa.
Guterres amesema katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa X kuwa ukiukaji huo wa sheria ya kimataifa unapaswa kukoma sasa.
SOMA : Guterres aonya upotevu wa amani
Jeshi la Israel lilithibitisha mashambulizi hayo jana Alhamisi, likisema lilifanya shambulio la usahihi dhidi ya magaidi wa Hamas waliokuwa ndani ya kituo hicho.



