Mpox yabisha hodi Morocco

MOROCCO : MTU mmoja amegundulika na virusi vya homa ya nyani(MPOX) katika jiji la Marrakesh nchini Morocco.

Mtu huyo ambaye atakuwa wa kwanza  ambaye anadaiwa kuwa virusi vya homa  ya nyani tangu mlipuko huo utangazwe katika nchi za Bara la Afrika na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hivi sasa mtu huyo bado anaendelea kupatiwa matibabu licha ya mamlaka za afya nchini humo kuendelea kumchunguza.  SOMA : Tanzania kudhibiti Mpox

Hatahivyo mamlaka zinaendelea kuwasiliana na watu wengine waliowasiliana nae  kabla hajapatiwa matibabu ili kudhibiti maambukizi yasiweze kuenea kwa wengine nchini humo.

Mpox inaweza kuenezwa kwa kukutana karibu na mtu aliyeambukizwa na pia kuenea kwa kugusa vitu ambavyo vimeambukizwa na virusi, kama vile matandiko, nguo na taulo.

Habari Zifananazo

Back to top button