Rwanda Congo wakubaliana kumaliza mivutano

ANGOLA :  JAMHURI ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda zimeridhia na kusaini waraka maalum wa kuimarisha amani katika eneo linalokabiliwa na machafuko la mashariki mwa Congo.

Tangu mwaka 2021, kundi la waasi M23  liliamua kuteka na kulidhibiti eneo la mashariki mwa Congo na kuwalazimu maelfu ya watu  kuyakimbia makazi yao na kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika eneo hilo.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje nchini Angola imedai kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa hayo mawili wamekubaliana kuanzisha chombo maalum kitakachoweka masharti ya kuhakikisha wanajeshi wa Rwanda wanaondoka katika ardhi ya Congo.

Hata hivyo taarifa hiyo ya serikali ya Angola haikutoa taarifa zozote kuhusiana na taratibu zitakazopitishwa. Soma: Congo Rwanda kusitisha mapigano

Rasimu ya awali ya mpango huo ya mwezi Agosti imeanisha kuhusu kuvunjiliwa mbali kundi la waasi lililoasisiwa na viongozi wa zamani wa jamii ya Wahutu waliohusika na mauaji ya halaiki ya Rwanda ya mwaka 1994 kama sharti muhimu la Rwanda kuwaondoa wanajeshi wa Rwanda.

Habari Zifananazo

Back to top button