Congo Rwanda kusitisha mapigano

CONGO : MAWAZIRI wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda wamethibitisha haja ya pande zinazozozana kuheshimu makubaliano ya usitishaji mapigano mashariki mwa Congo.

Wawakilishi wa Congo na Rwanda walikutana na waziri wa mambo ya nje wa Angola Tete Antonio mjini Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Congo, karibu na mpaka kati ya Congo na Rwanda kuzindua kamati ya kufuatilia ukiukaji wa makubaliano ya kusitishwa kwa vita.

Katika kikao hicho, Antonio amesema ni lazima pande hizo mbili ziheshimu  makubaliano hayo yenye lengo la kutafuta muafaka wa amani kati ya nchi hizo mbili.

Advertisement

Kwa upande wake, waziri wa mambo ya nje wa Congo Therese Kayikwamba Wagner, hakutoa tamko lolote baada ya mkutano huo.

SOMA: Kitengo kusitisha vita Congo kimezinduliwa

Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe, amesema nchi yake bado iko katika mchakato wa kutafuta amani.

Kamati hiyo ya kufuatilia usitisahji wa mapigano itaongozwa na Angola na kujumuisha wawakilishi kutoka Congo na Rwanda.