CONGO : KITENGO cha kufuatilia makubaliano ya kusitisha vita kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda M23, kimezinduliwa.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Angola ilisema kuwa itaongoza kitengo hicho cha kufuatilia mkataba wa kusitisha mapigano Kongo kitakachowajumuisha maafisa wa Kongo na Rwanda.
Waasi wa M23 wengi wao wanadaiwa kutoka kabila la Watutsi ambao wameteka maeneo kadhaa ya mashariki mwa Kongo inayokabiliwa na ghasia tangu mwaka 2021 na kuwalazimu maelfu ya watu kukimbia makazi yao huku wengine wakitaabika na upatikanaji wa huduma za kibinadamu.
Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliwa saini mwezi Agosti na yaliweza kuleta utulivu lakini tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba, kundi hilo la M23 liliendelea kufanya mashambulizi katika jimbo la Kivu Kaskazini.
Comments are closed.