Tanesco yafafanua kukatika kwa umeme asubuhi hii

DODOMA: MIKOA iliyounganishwa na Gridi ya Taifa imekosa umeme ikisababishwa na hitilafu katika Mfumo wa Gridi ya Taifa iliyotokea saa 04:03 asubuhi ya leo.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika taarifa yake kwa umma imeeleza kuwa wataalamu wao wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha hitilafu hiyo.

“Umeme kwa sasa umeanza kurejea kwa awamu katika Mikoa iliyokuwa inakosa umeme na jitihada zinaendelea kuhakikisha Mikoa yote inapata umeme mapema iwezekanavyo,” imeeleza taarifa hiyo.

Katika taarifa hiyo Tanesco limewaomba radhi wateja wao kwa walichoeleza usumbufu uliojitokeza.

“Shirika litaendelea kutoa taarifa za hali ya urejeshaji wa huduma ya umeme kwa kadri hali inavyoimarika,” imefafanua.

Habari Zifananazo

Back to top button