Rais Putin ateua gavana mpya

URUSI : RAIS wa Urusi Vladimir Putin amemteua gavana mpya wa mkoa wa Kursk, Alexander Khinshtein.
Alexander Khinshtein, mwandishi wa habari aliyeingia bungeni mwaka 2003, anachukuwa nafasi ya Alexei Smirnov, ambaye alishikilia nafasi hiyo mwezi Mei akiungwa mkono na Ikulu ya Kremlin.
Mapema mwaka huu, jeshi la Ukraine lilifanya uvamizi wa kushtukiza dhidi ya mkoa wa Kursk, na kupelekea Urusi kuingia hasara kubwa.
Uteuzi wa Khinstein unachukuliwa na wengi kama ishara ya mageuzi makubwa kwenye mfumo wa ulinzi wa Urusi hasa ukizingatia Khinstein alikuwa mshauri mkuu katika kikosi maalum cha ulinzi wa Rais Putin.
Hatahivyo, vikosi vya Urusi bado vinaendelea kuwaondosha wanajeshi wa Ukraine kwenye mkoa wa Kursk kwa miezi kadhaa sasa. SOMA : Jeshi la Korea Kaskazini laingia Urusi
Kwa mujibu wa duru za kijasusi za kimagharibi zinaeleza kuwa wanajeshi wa Korea Kaskazini wamekuja kwa ajili ya kuongeza nguvu kukomboa mkoa huo uliokuwa sehemu ya eneo la Ukraine.



