URUSI : Msemaji wa Pentagon, Meja Jenerali Pat Ryder amesema kati ya wanajeshi 11,000 na 12,000 kutoka Korea Kaskazini tayari wamewasili nchini Urusi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwa mujibu wa data za kijasusi zinaeleza kwamba wanajeshi 11,000 wa Korea Kaskazini wako katika eneo la Kursk ambalo vikosi vyake vya kijeshi vinaendesha operesheni za kijeshi dhidi ya jeshi la Urusi.
Moscow haijakana kuhusu madai ya kuwepo kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi lakini bado haijaweka bayana jinsi gani wamejipanga kuwatumia.
Hatahivyo, Nchi za Magharibi zimedai kuwa matumizi ya wanajeshi wa Korea Kaskazini kutazidisha mzozo wa kivita kati ya Urusi na Ukraine.
SOMA: Urusi kujadiliwa uvamizi Ukraine