BERLIN : RAIS wa Marekani Joe Biden amewasili mjini Berlin kwa ziara ya kikazi kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wengine wakubwa kutoka Ujerumani, Ufaransa na Uingereza.
Katika kikao hicho,watajadili pia mgogoro wa Mashariki ya Kati ambao utakuwa ni ajenda kuu ya mazungumzo.
Hatahivyo wamesema mauaji ya Israel dhidi ya kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar yanaweza pia kuleta tija katika usitishaji vita huko Gaza.
Wakatihuohuo,Ukraine imeendelea kuwaomba washirika wake kuchukua hatua za haraka za kusitisha mapigano ya vita nchini Ukraine. SOMA: Urusi yasitisha mkataba wa nyuklia na Marekani