Dk Biteko mgeni rasmi tamasha Ijuka Omuka

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha La Ijuka Omuka linalolenga kuwakutanisha wazaliwa wa Kagera wanaoishi ndani na nje ya nchi kujadili fursa za uwekezaji zilizoko mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa akizungumza na vyombo vya habari amesema tamasha hilo litaanza Desemba 18-26 kwa kujumuisha maonesho makubwa ya kibiashara na kutambulisha utamaduni halisi wa wakazi wa Kagera.

Amesema ufunguzi wa tamasha hilo utafanyika Desemba 19 ambapo wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watajadili fursa za uwekezaji katika sekta za ujenzi wa viwanda na utalii katika na kuangalia namna Kagera inavyoweza kurudi katika uchumi wake kama miaka ya zamani

“Mwaka Jana tulifanya Ijuka Omuka na mpaka sasa kuna mafanikio japo haikuwa  ya watu wengi ,mwaka huu tunatizamia kufanya maonyesho makubwa yenye vionjo mbalimbali kama kukutanisha wadau wakubwa sana  kujadili kwa upana na kuangalia namna ya kuinua mkoa kiuchumi kwa namna moja au nyingine,” amesema Mwassa.

Aidha amesema tamasha hilo litagubikwa na burudani nyingi kutoka kwa wasaniii pamoja na utamaduni wa mapishi  ya vyakula vya asili ambavyo vimesahaurika kama ukumbusho wa utamaduni halisi wa wakazi wa Kagera.

Habari Zifananazo

Back to top button