Rais Yoon hatarini kuondolewa madarakani Korea Kusini
BUNGE la Korea Kusini leo limepiga kura kumuondoa madarakani Rais Yoon Suk Yeol wa nchi hiyo kufuatia tangazo lake la amri iliyodumu muda mfupi ya kutangaza sheria ya kijeshi.
Hatua hiyo ya Bunge imepongezwa na umati wa watu waliokuwa wakishangilia, wakielezea matokeo hayo kama tukio la kidemokrasia yenye ustahimilivu ya taifa hilo.

Bunge la Taifa limepiga kura 204 kuunga mkono Rais kuondolewa wakati kura 85 zimekataa.
Mamlaka na majukumu ya urais ya Yoon yatasimamishwa, na afisa namba mbili wan chi hiyo Waziri Mkuu, Han Duck-soo, atachukua nafasi ya mamlaka yake mara tu nakala za hati ya kumuondoa madarakani zitakapowasilishwa kwa Yoon na pia Mahakama ya Kikatiba.

Mahakama ina muda wa hadi siku 180 kuamua iwapo itamwondoa Yoon kama rais au itamrejeshea mamlaka yake.
Iwapo ataondolewa madarakani, uchaguzi wa kitaifa kurithi nafasi yake lazima ufanyike ndani ya siku 60.
Hiyo ni mara ya pili kwa Bunge la Kitaifa kupiga kura kuhusu hoja ya kumuondoa Yoon madarakani.


