Ateba awapa raha Simba

DAR ES SALAAM: MABAO mawili ya mshambuliaji Leonel Ateba leo yameiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ken Gold mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam.
Kutokana na matokeo hayo Simba imefikisha alama 31 ikishika nafasi ya pili nyuma ya Azam yenye alama 33 kwa michezo 15. Simba imecheza mechi 12.



