RCC yapokea mapendekezo kufutwa mji wa Ngaramtoni

KIKAO cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC)  kimepokea mapendekezo kutoka Halmashauri ya Arusha DC ya kufutwa kwa Mamlaka ya Maji mdogo wa  Ngaramtoni uliopo Halmashauri hiyo kutokana na gharama za uendeshaji

Akiwasilisha mapendekezo hayo kwenye kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Suleiman Msumi amesema uamuzi huo unatokana na malalamiko ya wananchi ambao wamedai  gharama ya huduma za uendeshaji wa Mamlaka ya mji huo mdogo kuwa kubwa

Amesema malalamiko hayo yalitolewa kwenye mikutano mbalimbali ya hadhara ikiwemo iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda aliyembatana na Mwenyekiti wa  Chama cha Mapinduzi Mkoa wa (CCM) kwaajili ya kusikiliza kero mbalimbali ,ambapo wananchi walilalamikia gharama za uendeshaji wa Mamlaka ya mji mdogo na kuomba ifutwe.

Halmashauri ilipokea malalamiko ya wananchi ambao walionyesha kuwa hawakotayari kuwepo kwa Mamlaka ya mji mdogo hivyo ilibidi halmashauri kuendesha mchakato wa vikao vya maoni kuanzia ngazi za vijiji na hatimaye kuwasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya fedha cha baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya pia kufikishwa kwenye kikao cha ushauri cha Wilaya.

Msumi alisema baada ya vikao hivyo kutoa mapendekezo halmashauri inayawasilisha kwenye kikao hicho muhimu cha ushauri cha mkoa ili yapelekwe Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi )kwa hatua za kutangazwa kwenye gazeti la serikali.

Akichangia hoja hiyo,Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Karatu,John Maha,ameomba halmashauri zao zipandishwe hadhi na kuwa manispaa  kwa kuwa kuna  faida zikipandishwa hadhi na kuwa manispaa.

Ameshauri iundwe Kamati ya Mkoa itakayokuwa ikipendekeza halmashauri kupandishwa hadhi na kuongeza kuwa hata Karatu nao wana Mamlaka ya mji mdogo .

Habari Zifananazo

Back to top button