India yazungumzia amani, usalama BRICS

SHANGHAI : WAZIRI MKUU wa India, Narendra Modi, amethibitisha nafasi muhimu ya India katika uongozi wa kimataifa kupitia mkutano wa BRICS, ambapo aliangazia umuhimu wa umoja huu katika kubadilisha utaratibu wa dunia.
BRICS, inayojumuisha Brazil, Urusi, India, China, na Afrika Kusini, imekuwa na mchango mkubwa katika kutatua changamoto za kimataifa, ikiwemo mizozo ya mipaka na ukosefu wa usawa wa kiuchumi.
Katika mkutano huo, India imesisitiza ushirikiano wa kimataifa unaozingatia maslahi ya pande zote na kuweka mbele masuala ya amani, usalama na maendeleo endelevu.
Wakatihuohuo ametoa wito wa kusitisha mapigano katika ukanda wa Gaza na kuitisha mazungumzo ya amani katika nchi hizo mbili yatayoweza kumaliza mgogoro huo.
Kwa sasa India inaendelea kuwa kiongozi katika kubadilisha mfumo wa kifedha duniani kupitia Benki ya Maendeleo Mpya (NDB), ikiwa na lengo la kupunguza utegemezi kwa mifumo ya kifedha ya Magharibi.
Kwa upande wa mabadiliko ya tabianchi, Modi amesema serikali ya India imewekeza katika nishati mbadala, na kusema kuwa tayari imejizatiti kuwa kiongozi katika sekta ya nishati ya kijani.SOMA: BRICS inavyozidi kuvutia mataifa Amerika Kusini
Mkutano wa BRICS umeonesha wazi India ina nguvu kubwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa duniani.



