Vifo vya pombe vyaongezeka kwa asilimia 42% Uingereza

UINGEREZA: TAKWIMU zinaonyesha kuwa vifo vinavyosababishwa na unywaji wa pombe vinaongezeka  kwa asilimia 42% nchini Uingereza katika kipindi cha miaka minne .

Zaidi ya watu 8,200 walifariki kutokana na pombe mwaka 2023, ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na mwaka 2019.SOMA: Pombe zinaua seli za ubongo

Kaskazini Mashariki ya Uingereza imerekodiwa kuwa na viwango vya juu zaidi vya vifo vinavyohusiana na pombe. Wakati wa janga la COVID-19, vifo vilivyohusiana na pombe viliongezeka, huku baada ya kufungwa kwa baa, watu wengi waligeukia kununua pombe madukani na kunywa majumbani huku matajiri wakiongoza kwa unywaji wa pombe.

Wanaume, hasa wa umri wa miaka 55-74, ndio waathirika wakubwa, na vifo vyao vikitokana na magonjwa ya ini yanayohusiana na pombe, huku wengi wao wakifa kabla ya umri wa miaka 75.

Jumuiya ya unywaji pombe salama (AHA) inayowakilishwa na mashirika 60 yanayofanya kazi ya kupunguza madhara yanayosababishwa na pombe umetabiri  kutakuwa na ongezeka la vifo kutokana na unywaji wa pombe.

Habari Zifananazo

Back to top button