Uchunguzi mkali shambulio la gari Magdeburg
KIONGOZI wa Ujerumani Kansela, Olaf Scholz ameahidi kufanyika kwa uchunguzi baada ya gari kuparamia kundi la watu kwenye soko la Krismasi katika jiji la Magdeburg ambapo watu watano wamekufa akiwemo mtoto.

Maafisa wa jiji hilo wamesema zaidi ya watu 200 wamejeruhiwa katika shambulio hilo Desemba 20.
Mtuhumiwa wa shambulio ambaye ni daktari mwenye asili ya Saudi Arabia anayeishi Ujerumani mwenye umri wa miaka 50 anaaminika kufanya shambulio hilo peke yake.

Picha zimeonesha mtuhumiwa huyo akikamatwa eneo la tukio.
Chanzo: BBC News


