Wafungwa 6000 watoroka gerezani

MAPUTO : MKUU wa Polisi nchini Msumbiji, Bernadino  Rafael amesema wafungwa 6,000, wakiwemo 29 ambao walihukumiwa kwa ugadi, walitoroka katika Gereza Kuu la Maputo siku ya Krismasi wakati wa maandamano kufuatia ushindi wa chama tawala cha Frelimo.

Rafael amesema wafungwa 33 walikufa na wengine 15 walijeruhiwa wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama. SOMA: Wapinzani Msumbiji kuandamana kupinga uchaguzi

Maandamano hayo, yaliyofanywa na wafuasi wa mgombea aliyeshindwa Venancio Mondlane, yalisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya polisi na kuanguka kwa ukuta wa gereza.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Msumbiji Pascoal Ronda ameyahusisha machafuko hayo na mzozo wa matokeo ya uchaguzi, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitoa wito wa mazungumzo na kukomesha vurugu.

Wafungwa wengi waliotoroka tayari wamekamatwa tena.

Habari Zifananazo

Back to top button