Sultan Jamshid afariki dunia

MUSCAT:JAMSHID bin Abdullah, Sultani wa mwisho kuitawala Zanzibar na aliyeondolewa mamlakani kwa mapinduzi ya Januari 1964 amefariki dunia.

Jamshid amefariki hospitalini nchini Oman jioni ya jana Jumatatu, Disemba 30 akiwa na umri wa miaka 95.

Taarifa za kifo chake zimeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Oman na sababu ya kifo alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.

Jamshid  anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya kifalme jijini Muscat Oman.

Jamshid alichukua madaraka ya Usultani mwaka 1963 baada ya miezi mitano alitawazwa kuwa Sultani wa Zanzibar. SOMA :  Dkt Mwinyi akutana ujumbe Oman Zanzibar

Hata hivyo, uhuru huo haukubaliwa na wote visiwani Zanzibar, na kusababisha mapinduzi ya Januari 12 1964 ambayo yalitamatisha utawala wa Jamshid ambaye alikaa madarakani kwa miezi sita tu.

Baada ya kupinduliwa kwa serikali ya kisultani, Jamshid alikimbilia uhamishoni, awali nchini Oman ambapo hakupewa hifadhi na hatimaye alielekea nchini Uingereza.

 

Habari Zifananazo

Back to top button