Urusi yatungua droni 22 za Ukraine

URUSI : WIZARA ya Ulinzi ya Urusi imetangaza kutunguliwa kwa ndege zisizo na rubani 22 za Ukraine katika maeneo sita ya Urusi, ikiwa ni pamoja na maeneo yaliyo mbali na mipaka ya Ukraine.

Kwa mujibu wa ujumbe wa mitandao ya kijamii wa wizara hiyo, ndege 10 zilidunguliwa katika eneo la Bryansk, nne kila moja katika mikoa ya Oryol na Rostov, mbili katika mkoa wa Belgorod, na droni moja kila moja katika mikoa ya Volgograd na Lipetsk.

Katika mji mkuu wa Kyiv, nyumba ya kibinafsi iliwaka moto baada ya kuangukiwa na uchafu kutoka kwa droni iliyoungua. Mkuu mpya wa utawala wa kijeshi wa Kyiv, Timur Tkachenko, alisema kuwa moto huo uliozuka katika wilaya ya Darnitsky tayari umedhibitiwa.

SOMA: Urusi yajipanga kudungua drone za Ukraine

Aidha, droni nyingine ya kamikaze ya Urusi ilitunguliwa katika wilaya ya Goloseevsky, kusini mwa Kyiv, kulingana na meya wa mji huo, Vitaliy Klitschko.

 

Habari Zifananazo

Back to top button