URUSI : JESHI la Anga la Urusi limetangaza kuharibu droni 54 zilizorushwa na Ukraine usiku kucha zikilenga maeneo matano ya Urusi.
Nusu ya droni hizo zilidunguliwa katika anga ya eneo la mpakani la Kursk huku nyengine zikiangushwa katika maeneo ya Bryansk, Smolensk, Oryol na Belgorod.
Kwa mujibu wa maafisa wa Urusi wamedai kuwa shambulizi hilo la droni lilisababisha kuzuka kwa moto mkubwa na kulazimisha watu walioko karibu na mji wa Toropets kuhamishwa na kupelekwa katika maeneo salama.
SOMA: Ukraine yaitaka Urusi mazungumzo ya amani