PSG, Barcelona zawania saini ya Jhon Duran

MABINGWA watetezi wa Ligue 1, Paris Saint-Germain inavutiwa kumsajili Jhon Duran wa Aston Villa na inaaminika klabu hiyo ya Ligi Kuu England inaweza kushawishika kumuuza mshambuliaji huyo wa Colombia mwenye umri wa miaka 21 kwa pauni milioni 60. (Talksport)

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco, tayari amekutana na wawakilishi wa Duran kwa ajili ya mazungumzo yasiyo rasmi ili kumfahamisha mshambuliaji wa Aston Villa kwamba yuko kwenye rada ya klabu hiyo ya Catalonia. (Sport)

Bayern Munich inataka kuipiku Manchester United katika kumsajili mshambuliaji wa Sweden, Viktor Gyokeres, mwenye umri wa miaka 26 anayekipiga klabu ya Sporting. (Star)

Ligi kuu ya kulipwa ya Saudi Arabia ina matumaini ya kumsajili kiungo wa Brazil Casemiro, 32, kutoka Manchester United mwezi huu. (Telegraph)

Manchester United na Tottenham zipo katika harakati za kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa, Randal Kolo Muani, kwa mkopo kutoka Paris St-Germain mwezi huu, huku Juventus pia ikionesha nia kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Athletic)

Habari Zifananazo

Back to top button