Trump akosolewa kuhusu kuichukua Canada

MAREKANI : RAIS mteule wa Marekani, Donald Trump, amezua mjadala mkubwa wa kimataifa baada ya kuzungumzia uwezekano wa kuuchukuwa Mfereji wa Panama, kisiwa cha Greenland, na hata kuigeuza Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Florida, Trump alieleza kuwa hawezi kukanusha uwezekano wa kutumia nguvu za kiuchumi au kijeshi kuchukua udhibiti wa Mfereji wa Panama na Greenland.

Trump alikosoa vikali utumiaji wa bidhaa za Canada na msaada wa kijeshi wa Marekani kwa nchi hiyo, akidai kuwa mpaka kati ya Marekani na Canada ni wa “kubuni.”

Aliongeza kuwa Marekani inaweza kutumia shinikizo la kiuchumi ikiwa Denmark itakataa kuuza Greenland kwa Marekani. SOMA: Trump kuwashughulikia waliobadili jinsia

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, alijibu kauli hiyo kwa kukosoa vikali mtazamo wa Trump, akisema kuwa hakuna nafasi ya kuanzishwa kwa mabadiliko yoyote kwenye uhusiano wa nchi hizo.

Kwa upande mwingine, serikali ya Panama ilieleza kuwa haitatoa mamlaka yake kwa Marekani, huku Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen, akisisitiza kuwa kisiwa cha Greenland hakiko kwenye mnada.

Habari Zifananazo

Back to top button