Umoja wa Mataifa kutafuta dola milioni 910 kusaidia Nigeria

NIGERIA : UMOJA wa Mataifa unatafuta dola milioni 910  ili kutoa msaada wa kibinadamu kwa watu kaskazini mwa Nigeria, ambao wanakabiliwa na changamoto kubwa za kibinadamu.

Hali hiyo inatokana na migogoro ya waasi ambayo imeendelea tangu mwaka 2009, pamoja na mafuriko mabaya yaliyotokea mwaka uliopita.

Takriban watu milioni 7.8 wanahitaji msaada wa kiutu katika majimbo matatu ya Adamawa, Borno, na Yobe.

Umoja wa Mataifa unalenga kuwasaidia watu milioni 3.6 kati yao. SOMA: Mafuriko yaua 30 Nigeria

Ripoti ya pamoja ya serikali ya Nigeria na Umoja wa Mataifa ya Novemba mwaka jana ilisema kuwa nchi inakabiliwa na mzozo mkubwa wa njaa duniani, huku zaidi ya watu milioni 30 wakitarajiwa kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula mwaka huu.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali mbaya kaskazini mashariki mwa Nigeria inazidi kusahaulika, huku mizozo mingine duniani kama vile vita huko Ukraine, Gaza na Sudan vikivutia umakini wa kimataifa.

 

Habari Zifananazo

Back to top button