Utawala wa kiraia kurejea Aprili Gabon

GABON : SERIKALI ya mpito nchini Gabon imesema itafanya uchaguzi wa rais Aprili 12, hii ikiwa ni hatua muhimu ya kuurejesha upya utawala wa kiraia baada ya mapinduzi yaliyohitimisha udhibiti wa miongo kadhaa wa familia ya Bongo.
Msemaji wa serikali ya Gabon Serapin Akure Davain ametoa tangazo hilo mapema hii leo baada ya mkutano wa baraza la mawaziri. SOMA: Kiongozi wa kijeshi Gabon aapishwa kuwa rais
Taifa hilo la Afrika lenye utajiri wa mafuta ambalo limetawaliwa na familia ya Bongo kwa miaka 55, ilipitisha katiba mpya katika kura ya maoni ya mwezi Novemba.
Rais wa mpito Jenerali Brice Oligui Nguema, aliyechukua wadhifa huo mara baada ya mapinduzi ya Agosti 2023, ameweka wazi azma yake ya kusalia madarakani.



