Miundombonu ya michezo miaka 4 ya Dk Samia

KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dk Samia Suluhu Hassan, Serikali imeongeza ufadhili, kuboresha miundombinu ya kisasa na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, hatua ambazo zimeleta mafanikio makubwa katika sekta ya michezo.

Miongoni mwa mafanikio hayo ni ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Benjamin Mkapa uliogharimu shilingi bilioni 31.

Aidha, mengine ni ujenzi wa uwanja mpya wa michezo mkoani Arusha unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 338 hadi kukamilika kwake.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Neema Msitha, amebainisha hayo leo Februari 18 ijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita katika sekta ya michezo kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia.

Amesema kuwa ujenzi wa uwanja mpya wa michezo jijini Dodoma unatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa gharama ya shilingi bilioni 310.

Vilevile, serikali inaendelea na ujenzi wa viwanja mbalimbali vya mazoezi, vikiwemo Gymkhana, Leaders Club, TIRDO, Law School na Uwanja wa Farasi, ambapo jumla ya shilingi bilioni 21 zitatumika hadi kukamilika kwa miradi hiyo.

Msitha amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya michezo ili kukuza vipaji na kuimarisha sekta hiyo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuinua maendeleo ya michezo nchini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button