Serikali yadhamiria kupanua fursa wanafunzi elimu ya amali

ZAIDI ya shilingi Bilioni nne zimetumika kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule za Sekondari 25 za Serikali zinazotoa elimu ya amali.
Akizungumza katika Mkutano wa Pamoja wa Tathimini ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu, Mkurugenzi Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Maulid Mnonya amesema katika shule hizo zinazotoa mafunzo ya amali, zina idadi ya wanafunzi 2,000 ambapo kati yao 184 ni wenye mahitaji maalum.
Amebainisha kuwa katika mkondo wa amali kuna fani kuu 15 na fani ndogondogo 75.
Lengo la serikali ni kuhakikisha baada ya miaka 10 kutoka mwaka huu kuwe na wanafunzi asilimia 30 kwenye mkondo wa amali na katika kutekeleza hilo shule 103 za amali ambapo kwa mwaka huu shule 29 zipo katika hatua za mwisho kukamilika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button