“Sitaki uchokozi” Kim Jong Un

KOREA KASKAZINI : SERIKALI ya Korea Kaskazini imelaani Marekani kwa kile ilichokiita uchokozi wa kisiasa na kijeshi, kufuatia kuwasili kwa meli ya ndege za jeshi la majini la Marekani katika bandari ya Busan, Korea Kusini.

Kim Yo Jong, dada wa kiongozi Kim Jong Un, alisema kuwa Marekani imeongeza uchokozi dhidi ya Korea Kaskazini tangu kuingia madarakani kwa utawala mpya mwaka huu, na kuendeleza sera ya uhasama ya utawala wa zamani.

Kim Yo Jong alisisitiza kuwa ikiwa Marekani itaendeleza uchokozi wake wa kijeshi, Korea Kaskazini itachukua hatua za kinga za kimkakati.

Aliongeza kuwa hatua hiyo itakuwa ni njia ya kulinda usalama wa taifa, huku akitahadharisha kuwa hali hiyo inaweza kuzua migogoro zaidi.SOMA: Jeshi la Korea Kaskazini laingia Urusi

Hata hivyo, Marekani imesema kuwa ziara ya meli hiyo ni ishara ya kujitolea kwake kwa usalama wa eneo la Asia na kuimarisha uhusiano na Korea Kusini.

Serikali ya Marekani imeongeza kuwa ziara hiyo inalenga kuongeza ushirikiano katika masuala ya kijeshi na kuimarisha uthabiti katika kanda hiyo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button